Friday, 3 February 2017
Raisi amteua Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu mkuu wa majeshi ya ulinzi [JWTZ]
Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dr John Magufuli amemwapisha Lutenia Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) pamoja na kuwateua maafisa wakuu wengine wa jeshi kushika nyadhifa mbalimbali.
Luteni Jenerali Venance Mabeyo ameshika nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Ndomba ambaye alistaafu Disemba 31, mwaka
Akizungumzia uteuzi wa maafisa wakuu walioteuliwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange amesema maafisa hao ni pamoja na Meja Jenerali James Mwakibolwa ambaye amekuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Nchi kavu kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Meja Jenarali Salum Mustafa Kijuu, Meja Jenerali Yakub Sirakwi anakuwa Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Gaudence Milanzi ambaye amateuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
Wengine walioteuliwa na Rais ni aliyekuwa afisa mnadhimu katika makao makuu kamandi ya Jeshi la Anga Brigedia Jenerali George Ingram ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kamandi hiyo, Brigedia Jenerali Jacob Kingu amekuwa Mkuu wa Shirika la Mzinga.
Brigedia Jenerali Robinson Mwanjela amekuwa Mkuu wa Chuo cha tiba Lugalo, Brigedia Jenerali George Msongole amekuwa Kamanda wa Brigedi ya Tembo na Brigedia Jenerali Sylvester Minja ambaye amekuwa Mkuu wa chuo cha Ukamanda na unadhimu na wote wameshika nafasi zilizoachwa wazi baada ya waliokuwa wakishika nyadhifa hizo kustaafu
Akizungumzia uteuzi wa maafisa wakuu walioteuliwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange amesema maafisa hao ni pamoja na Meja Jenerali James Mwakibolwa ambaye amekuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Nchi kavu kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Meja Jenarali Salum Mustafa Kijuu, Meja Jenerali Yakub Sirakwi anakuwa Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Gaudence Milanzi ambaye amateuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment